26
Hotuba Ya Tisa Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Utukufu Wa Mungu Hauchunguziki
Kisha Ayubu akajibu:
“Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo!
Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!
Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima?
Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha!
Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo?
Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?
 
“Wafu wako katika maumivu makuu,
wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake.
Mauti* Yaani Kuzimu; Kiebrania ni Sheol. iko wazi mbele za Mungu;
Uharibifu Kwa Kiebrania ni Abadon. haukufunikwa.
Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu;
naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu.
Huyafungia maji kwenye mawingu yake,
hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
Huufunika uso wa mwezi mpevu,
akitandaza mawingu juu yake.
10 Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji,
ameweka mpaka wa nuru na giza.
11 Nguzo za mbingu nazo zatetemeka,
zinatishika anapozikemea.
12 Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari;
kwa hekima yake alimkata Rahabu Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani, mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. vipande vipande.
13 Aliisafisha anga kwa pumzi yake;
kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.
14 Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake;
tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu!
Ni nani basi awezaye kuelewa
ngurumo za nguvu zake?”

*26:6 Yaani Kuzimu; Kiebrania ni Sheol.

26:6 Kwa Kiebrania ni Abadon.

26:12 Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani, mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.