3
1 Sasa hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa kwake huko Hebroni: mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu kutoka Yezreeli; wa pili alikuwa Danieli, kwa Abigaili kutoka Karmeli; 2 watatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa ni Maaka, binti wa Talmai mfalme wa Geshuri. Wanne alikuwa ni Adoniya mwana wa Hagithi; 3 watano alikuwa ni Shefatia kwa Abitali, wasita alikuwa ni Ithraeamu kwa Egla mkewe. 4 Hawa sita walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni, alipo tawala miaka saba na miezi sita. Kisha akatawala miaka thelathini na mitatu huko Yerusalemu. 5 Hawa wana wa nne, kwa Bathshua binti wa Amieli, walizaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Nathani, na Sulemani. 6 Wana tisa wengine wa Daudi walikuwa ni: Ibhari, Elishua, Elipeleti, 7 Noga, Nefegi, Yafia, 8 Elishama, na Elifeleti. 9 Hawa walikuwa wana wa Daudi, pasipo kuwehesababu wana wa masuria wake. Tamari alikuwa dada yao. 10 Mwana wa Sulemani alikuwa ni Rehoboamu. Mwana wa Rehoboamu alikuwa Abiya. Mwana wa Abiya alikuwa Asa. Mwana wa Asa alikuwa Yehoshafati. 11 Mwana wa Yehoshafati alikuwa Yoramu. Mwana wa Yoramu alikuwa Ahazia. Mwana wa Ahazia alikuwa Yoashi. 12 Mwana wa Yoashi alikuwa Amazia. Mwana wa Amazia alikuwa Azaria. Mwana wa Azaria alikuwa Yothamu. 13 Mwana wa Yothamu alikuwa Ahazi. Mwana wa Ahazi alikuwa Hezekia. Mwana wa Hezekia alikuwa Manase. 14 Mwana wa Manase alikuwa Amoni. Mwana wa Amoni alikuwa Yosia. 15 Wana wa Yosia aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza ni Yohana, wapili Yehoyakimu, mwanae watatu Sedekia, na mwanae wanne Shalumu. 16 Wana wa Yehoyakimu walikuwa Yehoyakini na Sedekia. 17 Wana wa YehoYakini, mateka, walikuwa Shealtieli, 18 Malkiramu, Pedaya, Shenezari, Yekamia, Hoshama, na Nedabia. 19 Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Wana wa Zerubabeli walikuwa Meshulamu na Hanania; Shelomithi alikuwa dada yao. 20 Wanae watano walikuwa Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia, na Yushabu Hesedi. 21 Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Mwanawe alikuwa Refaya, na uzao wake zaidi walikuwa ni Arnani, Obadia, na Shekania. 22 Mwana wa Shekania alikuwa Shemaya. Wana wa Shemaya walikuwa Hatushi, Igali, Baria, Nearia, na Shafati. 23 Wana watatu wa Nearia walikuwa Elioenai, Hizekia, na Azrikamu. 24 Wana saba wa Elioenai walikuwa Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohana, Delaya, na Anani.