22
Basi Daudi aliondoka hapo na akatoroka kwenda kwenye pango la Adulamu. Kaka zake na wote wa nyumba ya baba yake waliposikia hayo, wakateremka kumwendea huko. Kila mmoja aliyekuwa na mahangaiko, kila mmoja aliyekuwa na deni, na kila mmoja ambaye hakuwa na furaha moyoni-wote walijikusanya kwake, na Daudi akawa jemedari wao. Kulikuwa na wanaume wapatao mia nne waliokuwa pamoja naye. Kisha Daudi alitoka huko akaenda Mispa huko Moabu. Akamwambia mfalme wa Moabu, “Tafadhali waruhusu baba na mama yangu wakae kwako hadi hapo nitakapojua kitu gani ambacho Mungu atafanya kwa ajili yangu.” Basi akawaacha kwa Mfalme wa Moabu. Baba na mama yake wakakaa na mfalme kwa muda wote ambao Daudi alikuwa kwenye ngome yake. Kisha nabii Gadi akamwambia Daudi, “Usikae tena katika ngome yako. Ondoka na uende katika nchi ya Yuda.” Kwa hiyo Daudi akatoka hapo na akaenda katika msitu wa Harethi. Sauli akasikia kwamba Daudi amepatikana, akiwa pamoja na watu aliokuwa nao. Wakati huo Sauli alikuwa akikaa Gibea chini ya mti wa mkwaju huko Rama, akiwa na mkuki wake mkononi mwake, na watumishi wake wote walikuwa wamesimama wamemzunguka. Sauli akawaambia watumishi wake, Sasa sikilizeni, watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya nyote kuwa majemedari wa maelfu na majemedari wa mamia, hata ninyi nyote mnapanga njama dhidi yangu? Hakuna hata mmoja wenu anayenijulisha kwamba mwanangu anafanya agano na mwana wa Yese. Hakuna hata mmoja wenu anayenionea huruma. Hakuna hata mmoja wenu anayenijulisha kwamba mwanangu anamchochea mtumishi wangu Daudi awe kinyume changu. Leo mejificha na ananisubiri ili anishambulie.” Kisha Doegi Mwedomu, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akajibu, Nilimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki mwana wa Ahitubu. 10 Alimwomba BWANA ili apate kumsaidia, na alimpatia mahitaji na upanga wa Goliathi, Mfilisti” 11 Kisha Mfalme akamtuma mtu amwite kuhani Ahimeleki mwana wa Ahitubu na watu wote wa nyumba ya baba yake, makuhani waliokuwa huko Nobu. Wote walifika mbele ya mfalme. 12 Sauli akasema, “Sasa sikiliza, mwana wa Ahitubu,” Naye akajibu, “Niko hapa, bwana wangu.” 13 Sauli akamwambia, “Kwa nini unapanga njama dhidi yangu, wewe pamoja na mwana wa Yese, kwa kumpatia mikate, na upanga, na umemwomba Mungu kusudi amsaidie Daudi, kusudi aniasi mimi, na kujificha sehemu ya siri, kama alivyofanya leo?” 14 Ndipo Ahimeleki akamjibu mfalme na kusema, “Je, ni nani miongoni mwa watumishi wako wote aliyemwaminifu kama Daudi, ni nani mkwe wa mfalme na yuko juu ya walinzi wako, na mwenye heshima nyumbani mwako? 15 Je, leo ni mara ya kwanza kwangu kumuomba Mungu apate kumsaidia? Hapana! Mfalme usinilaumu mimi mtumishi wako kwa jambo lolote wala jamaa zangu wote. Maana mimi mtumishi wako sijui lolote kuhusu kadhia hii.” 16 Mfalme akamjibu, “Hakika utakufa, Ahimeleki, wewe na jamaa yote ya nyumba ya baba yako.” 17 Mfalme akamwambia mlinzi aliyesimama karibu naye, “Geuka na uwauwe makuhani wa BWANA. Kwa sababu wanamuunga mkono Daudi, na sababu walijua kwamba alikimbia, lakini hawakunijulisha.” Lakini watumishi wa mfalme hawakunyoosha mkono wao kuwaua makuhani wa BWANA. 18 Ndipo mfalme akamwambia Doegi, “Geuka na uwauwe makuhani.” Hivyo Doegi Mwedomu akageuka na kuwapiga makuhani; akawaua watu themanini na watano waliovaa naivera ya kitani siku hiyo. 19 Kwa ncha ya upanga, aliupiga Nobu, mji wa makuhani, akiwaua wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ng'ombe na punda na kondoo. Wote aliwaua kwa ncha ya upanga. 20 Lakini mmoja wa wana wa Ahimeleki mwana wa Ahitubu, aliyeitwa Abiathari, aliponyoka na kukimbilia kwa Daudi. 21 Abiathari akamwambia Daudi kwamba Sauli amewaua manabii wa BWANA. 22 Daudi akamwambia Abiathari, “Nilifahamu kuwa siku hiyo, Doegi Mwedomu alikuwa mahali pale, kwamba hakika angemwambia Sauli. Nina wajibika kwa kifo cha kila mtu katika familia ya baba yako! 23 Kaa pamoja nami na usiogope. Maana mtu anayetafuta roho yako anatafuta pia roho yangu. Utakuwa salama ukiwa pamoja nami.”