3
Kwa hiyo, tulipo kuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tulifikiri kuwa ilikuwa vema kubaki kule Athene peke yetu. Tulimtuma Timotheo, ndugu yetu na mtumishi wa Mungu katika injili ya Kristo, kuwaimalisha na kuwafariji kuhusiana na imani yenu. Tulifanya haya ili kusudi asiwepo yeyote wa kuteteleka kutokana na mateso haya, kwa kuwa wenyewe mnajua kwamba tumekwisha teuliwa kwa ajili ya hili. Kwa kweli, wakati tulipokuwa pamoja nanyi, tulitangulia kuwaeleza ya kuwa tulikuwa karibu kupata mateso, na hayo yalitokea kama mjuavyo. Kwa sababu hii, nilipo kuwa siwezi kuvumilia tena, nilituma ilikusudi nipate kujua juu ya imani yenu. Huenda mjaribu alikuwa angalau amewajaribu, na kazi yetu ikawa ni bure. Lakini Timotheo alikuja kwetu kutokea kwenu na akatuletea habari njema juu ya imani na upendo wenu. Alitwambia ya kuwa mnayo kumbukumbu nzuri juu yetu, na kuwa mnatamani kutuona kama ambavyo nasi twatamani kuwaona ninyi. Kwa sababu hii, ndugu tulifarijika sana na ninyi kwa sababu ya imani yenu, katika taabu na mateso yetu yote. Kwa sasa tunaishi, kama mkisimama imara kwa Bwana, Kwani ni shukurani zipi tumpe Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha yote tuliyonayo mbele za Mungu juu yenu? 10 Tunaomba sana usiku na mchana ili tuweze kuziona nyuso zenu na kuwaongezea kinachopungua katika imani yenu. 11 Mungu wetu na Baba mwenyewe, na Bwana wetu Yesu atuongoze njia yetu tufike kwenu. 12 Na Bwana awafanye muongezeke na kuzidi katika pendo, mkipendana na kuwapenda watu wote, kama tunavyowafanyia ninyi. 13 Na afanye hivi ili kuiimarisha mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu wetu na Baba yetu katika ujio wa Bwana Yesu pamoja na watakatifu wake wote.