12
1 Ikawa kwamba, Rehoboamu alipokuwa ameimarishwa na mwenye nguvu, kwamba akaikataa sheria ya Yahwe—na Waisraeli wote pamoja naye. 2 Ilitokea katika mwaka wa tano wa Mfalme Rehoboamu, kwamba, Shishaki, mfalme wa Israeli, akaja kinyume na Yerusalelemu, kwa sababu watu walikuwa wameacha kuwa waaminifu kwa Yahwe. 3 Akaja na magari elfu moja na mia mbili pamoja naye na wapand farasi elfu sitini. Askari wasio hesabika wakaja pamaoja naye kutoka Misri: Walubi, Wasukii, na Waethiopia. 4 Akaiteka miji yenye ngome ya Yuda na akaja Yerusalemu. 5 Sasa Shemaya nabii akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda ambao walikuwa wamekusanyika pamoja Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki. Shemaya akasema kwao, “Hivi ndivyo anavyosema Yahwe: Mmenisahau, kwa hiyo pia nimewaweka katika mkono wa Shishaki”. 6 Kisha wakuu wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, “Yahwe ni mtakatifu.” 7 Yaahwe alipoona kuwa wamejinyenyekeza, neno la Yahwe likamjia Shemaya, likisema, “Wamejinyenyekeza. Stawaadhibu; nitawaokoa kwa hataua fulani, na hasira yangu haitamiminwa juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki. 8 Vile vile, watakuwa watumishi wake, ili kwamba wajue nini maana ya kunitumikia mimi na kuwatumikia watawala wa nchi zingine.” 9 Kwa hiyo Shishaki, mfalme wa Misiri akaja Yerusalemu akazichukua hazina katika nyumba ya Yahwe, na hazina katika nyumba ya mfalme. akachukua kila kitu; pia akazichukua ngao za dhahabu alizokuwa amezitengeneza Selemani. Mfalme 10 Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba katika nafasi zake na kuzikabidhi mikoni mwa maamrijeshi wa walinzi, amabao waliilinda milango ya kuelekea kwenye nyumba ya mfalme. 11 Ikawa kwamba mfalme kila alipoingia katika nyumba ya Yahwe, walinzi wakazibeba; kisha wakazirudisha katika nyumba ya ulinzi. 12 Rehoboamu alipojinyenyekeza mwenyewe, ghadhabu ya Yahwe ikampisha mbali, kwa hiyo hakumwangamiza kabisa kabisa; pembeni, bado kulikuwa na baadhi ya wema wa kupatikana katika Yuda. 13 Hivyo mfalme Rehoboamu akafanya ufalme wake imara katika Yerusalemu, na kwa hiyo akatawala. Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka aroabaini na moja alipoanza kutawala, na akatawala kwa muda wa mika kumi na saba katika Yerusalemu, mji ambao Yahwe alikuwa ameuchagua kutoka kwa makabila ya Israeli ili kwamba aliweke jina lake humo. Jina lake aliitwa Naama, Mwamoni. 14 Akafanya yaliyokuwa uovu, kwa sababu hakuuelekeza moyo wake kumtafuta Yahwe. 15 Kwa mambo mengine kuhusu Rehoboamu, mwanzo na mwisho, hayakuandikwa katika maandishi ya Shemaya nabii na ya Ido mwonaji, ambayo pia yana kumbukumbu ya vizazi na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu? 16 Rehoboamu akalala pamoja na babu zake na alizikwa katika mji wa Daudi; Abiya mwanye akawa mfalme katika nafasi yake.