12
1 Katika mwaka wa saba wa Yehu, utawala wa Yoashi ulianza; alitawala kwa mda wa miaka arobaini huko Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Sibia, wa Beersheba. 2 Yoashi akafanya yaliyo mema usoni mwa Yahwe siku zote, kwa sababu Yehoyada kuhani alimfundisha. 3 Lakini sehemu ya juu haikuchukuliwa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kuchoma ubani kwenye sehemu za juu. 4 Yoashi akamwambia kuhani, “Pesa zote zilizokuja kama sadaka takatifu kwenye nyumba ya Yahwe, pesa ya matumizi pesa ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na pesa yote aonayo moyoni mwake kuileta kwenye nyumba ya Yahwe- 5 makuhani watapokea pesa kutoka miongoni mwa mmoja wa watunza pesa na kutengeneza kila sehemu itakayoonekana imeharibika kwenye hekalu.” 6 Lakini kama mwaka wa ishirini na tatu wa mfalme Yoashi, makuhani hawakuwa wameandaa kitu chochote kwenye hekalu. 7 Mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani na kuhani mwingine; akawaambia, “Kwa nini hamjaandaa kitu chochote kwenye hekalu? Sasa msichukue tena pesa kutoka kwa walipa kodi wenu, lakini chukueni kile kilichokuwa kikikusanywa kwa ajili ya matengenezo ya hekalu na uwapatia wale wanaoweza kufanya matengenezo. 8 Hivyo makuhani wakakubaliana wasichukue pesa tena kutoka kwa watu na wasitengeneze wenyewe. 9 Badala yake, Yehoyada yule kuhani akachukua kasha, akatoboa tundu kwenye kifuniko chake, na kuliweka karibu na madhabahu, upande wa kulia kama mtu anaingia kwenye madhabahu ya Yahwe. Makuhani ambao walikuwa wakilinda mlango wa hekalu wakatumbukiza pesa zote ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe. 10 Ikawa walipoona kwamba kulikuwa na pesa za kutosha kwenye kasha, mwadishi wa mfalme na kuhani mkuu wakaja na kuweka pesa kwenye mifuko na kisha kuhesabu, pesa ikaonekana kwenye nyumba ya Yahwe. 11 Wakawapa pesa ambayo ilikuwa imepimwa kwenye mikono ya watu ambao waliokuwa wanatunza nyumba ya Yahwe. Wakawalipa mafundi seremala na wajenzi ambao walikuwa wemefanya kazi kwenye nyumba ya Yahwe, 12 na waashi na wakata mawe, kwa ajili ya kununua mbao na kukata mawe kwa ajili ya kutengenezea nyumba ya Yahwe, na yote iliyokuwa inahitajika kulipwa kwa ajili ya kuitengeneza. 13 Lakini ile pesa iliyokuwa imeletwa kwenye nyumba ya Yahwe haikulipwa kwa ajili ya vikombe vya fedha, mabeseni, au dhahabu au fedha yoyote ya vyombo. 14 Waliwapa hizi fedha wale ambao waliokuwa wamefanya kazi ya kutengeneza nyumba ya Yahwe. 15 Pia, hakukuhitajika zile pesa zilipwe kwa ajili ya matengenezo ili kuwajibika kwa kuwa watu walizipokea nakuzilipa kwa watenda kazi, kwa sababu hawa watu walikuwa waadilifu. 16 Lakini pesa kwa ajili ya matoleo ya hatia na pesa kwa ajili ya matoleo ya dhambi hazikuwa zimeletwa kwenye hekalu la Yahwe, kwa sababu zilikuwa mali ya makuhani. 17 Kisha Hazaeli mfalme wa Shamu akashambuliwa na kupigana dhidi ya Gathi, na kuichukua. 18 Ndipo Hazaeli akageuka kuishambulia Yerusalemu. Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vitu vyote ambavyo Yehoshefati na Yehoramu na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, na kuviweka wakfu, na vile alivyokuwa ameviweka wakfu, na dhahabu zote zilizokuwa zimeonekana kwenye gala la nyumba ya Yahwe na la mfalme akawatuma kwenda kwa Ahazi mfalme wa Shamu. Kisha Hazaeli akaenda zake kutoka Yerusamu. 19 Kama mambo mengine yanayomuhusu Yoashi, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? 20 Watumishi wake wakainuka na kupanga pamoja; wakamteka Yoashi katika Bethi Milo, kwenye njia ya kushukia kwa Sila. 21 Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakamshambulia na akafa. Wakamzika Yoashi pamoja na mababu zake katika mji wa Daudi, na Amazia, mtoto wake, akawa mfalme kwenye sehemu yake.