9
1 Kwa kuwa nilifikiri haya yote katika akili zangu kufahamu kuhusu watu wenye haki na wenye hekima na matendo yao. Wote wako katika mikono ya Mungu. Hakuna anayefahamu kama upendo au chuki itakuja kwa mtu. 2 kila mmoja ana mwisho sawa. Mwisho sawa una subiria watu wenye haki na waovu, wema, walio safi na wasio safi, yeye atoaye dhabibu na yule asiye dhabihu. Kama vile watu wema watakufa wenye dhambi nao watakufa vivyo hivyo. kama vile yule anayeapa atakavyo kufa, vivyo hivyo mtu yule aogopaye kuweka kiapo naye atakufa. 3 Kuna mwisho mwovu kwa kila kitu kinachofanyika chini ya jua, na mwisho kwa kila mtu. Moyo wa mwanadamu umejaa uovu, na wazimu uko katika mioyo yao wakati wanaishi. Hivyo baada ya hilo wanaenda kwa wafu. 4 Kwa kuwa yeyote anayeungana na wote walio hai kuna tumaini, kama vile mbwa aliye hai ni bora kuliko simba aliye kufa. 5 Kwa kuwa watu walio hai, lakini walio kufa hawajui chochote. Hawana tena tuzo yeyote kwa sababu kumbukumbu yao imesahaulika. 6 Upendo wao, chuki na wivu vimekatiliwa mbali muda mwingi. Hawatapata sehemu katika kitu chochote kinachofanyika chini ya jua. 7 Nenda zako, kula mkate wako kwa furaha, na kunywa mvinyo wako na moyo wa furaha, kwa kuwa Mungu huruhusu kusherehekea kazi njema. 8 Nguo zako ziwe nyeupe siku zote, na kichwa chako kipake mafuta. 9 Ishi kwa furaha na mwanamke umpendaye siku zako zote za maisha yako ya ubatili, siku ambazo Mungu amekupatia chini ya jua wakati wa siku zako za ubatili. Hiyo ni thawabu kwa ajili ya kazi yako chini ya jua. 10 Chochote mkono wako unakifanya, kifanye kwa nguvu zako kwa sababu hakuna kazi, au ufafanuzi au ujuzi au hekima katika Sheol, unapoenda. 11 Nimeona baadhi ya vitu vyakuvutia chini ya jua: Mashindano hayatokani na watu wenye mbio. Vita havitokani na watu imara. Mkate hautokani na watu wenye busara. Mali hazitokani na watu wenye ufahamu. Kibali hakitokani na watu wenye ujuzi. Badala yake muda na bahati huwaathiri wao wote. 12 Kwa kuwa hakuna anaye fahamu wakati wake wa kufa, kama vile samaki wanaswavyo katika nyavu ya kifo, au kama vile ndege akamatwavyo katika mtego. Kama wanyama wanadamu wamefungwa katika nyakati mbaya ambazo ghafla huwaangukia. 13 Pia nimeona hekima chini ya jua kwa namna ambayo kwangu ilionekana kubwa. 14 Kulikuwa na mji mdogo na watu wachache ndani yake, na mfalme mkuu akaja kinyume na mji huo na akauzingira na akajenga mahandaki kwa ajili ya kuushambulia. 15 Na katika mji kulikuwa na masikini, mtu mwenye hekima, ambaye kwa hekima yake aliuokoa mji. Ila baadaye aliye mkumbuka yule masikini. 16 Hivyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu, lakini hekima ya mtu masikini hudharauliwa, na maneno yake hayasikilizwi.” 17 Maneno ya watu wenye hekima yaliongewa polepole yanasikiwa vizuri kuliko makelele ya mtawala yeyote miongoni mwa wapumbavu. 18 Hekima ni bora kuliko silaha za vita, lakini mwenye dhambi mmoja anaweza kuharibu mazuri mengi.