6
Kisha Yahweh akasema na Musa, “Sasa utaona nitakacho fanya kwa Farao. Utaona hili, kwa kuwa ata waacha waenda kwa mkono wangu hodari. Kwasababu ya mkono wangu hodari, ata waondoa nje ya nchi.” Mungu akasema na Musa na kumwambia, “Mimi ni Yahweh. Nilimtokea Ibrahimu, Isaka, na Yakobo kama Mungu mwenye nguvu; lakini kwa jina langu, Yahweh, sikujuliikana kwao. Pia niliimarisha agano langu na wao, ilikuwapatia nchi ya Kanani, nchi walioishi kama sio raia, nchi walio tanga tanga. Zaidi ya yote, nimesikia kilio cha Waisraeli ambao wa Misri wame wa chukua watumwa, na nimekumbuka agano langu. Kisha basi, sema kwa Waisraeli, 'Mimi ni Yahweh. Nitawatoa kwenye utumwa chini ya wa Misri, na kuwaweka huru na nguvu zao. Nitawaokoa kwa kudhihirisha nguvu zangu, na kwa matendo ya ajabu ya hukumu. Nitawaleta kwangu kama watu wangu, na nitakuwa Mungu wenu. Mtajua kuwa mimi ndiye Yahweh Mungu wenu, aliye watoa kwenye utumwa chini ya wa Misri. Nitawaleta kwenye nchi niliyo muahidi kumpa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Nitawapa kama mali yenu. Mimi ni Yahweh.”' Musa alipo waambia haya Waisraeli, hawakumsiliza kwasababu ya mateso magumu ya utumwa wao. 10 Hivyo Yahweh akazungumza na Musa na kumwambia, 11 “Nenda umwambie Farao, mfalme wa Misri, awaache watu wa Israeli waondoke kwenye nchi yake.” 12 Musa akamwambia Yahweh, “Kama Waisraeli hawajanisikiliza mimi, kwa nini Farao anisikillize mimi, tangu mimi sio mzuri wakuzungumza?” 13 Yahweh akasema na Musa na Aruni. Akawapa amri ya Waisraeli na Farao, mfalme wa Misri, awatoe Waisraeli kutoka nchi ya Misri. 14 Hawa walikuwa vichwa wa nyumba za baba yao: wana wa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa Hanoki, Palu, Hezroni, na Karmi. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Rubeni. 15 Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli - mwana wa mwanamke wa Kanani. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Simeoni. 16 Hapa yameorodheshwa majina ya wana wa Lawi, pamoja na uzo wao. Walikuwa ni Gerishoni, Kohathi, na Merari. Lawi aliishi mpaka alipo kuwa na miaka 137. 17 Wana wa Gerishoni walikuwa Libni na Shimei. 18 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na uzieli. Kohathi aliishi hadi miaka 133. 19 Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi. Hawa walikuja kuwa mababu wa ukoo wa Walawi, pamoja na uzao wao. 20 Amramu alimuoa Yokebedi, dada yake baba yake. Alimzalia Aruni na Musa. Amramu aliishi miaka 137 na akafa. 21 Wana wa Izhari walikuwa Kora, Nefegi, na Zikri. 22 Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elizafani na Sithri. 23 Aruni alimuoa Elisheba, binti wa Aminadabu, dada wa Nashoni. Alimzaa Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari. 24 Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasa. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Wakora. 25 Eleazari, mwana wa Aruni, alimuoa mmoja wa mabinti Wa Putieli. Alimzalia Fineazi. Hawa walikuwa vichwa wa nyumba za baba yao miongoni mwa Walawi, pamoja na uzao wao. 26 Hawa wanaume wawili walikuwa Musa na Aruni ambao Yahweh alisema, “Waleteni Waisraeli kutoka nchi ya Misri, kwa makundi ya wanaume wapiganaji.” 27 Aruni na Musa wakazungumza na Farao, mfalme wa Misri, awaruhusu Waisraeli watoke Misri. Hawa walikuwa Musa na Aruni wale wale. 28 Pale Yahweh alipo zungumza na Musa katika nchi ya Misri, 29 alimwambia, “Mimi ni Yahweh. Sema kwa Farao, mfalme wa MIsri, kila kitu nitacho kwambia.” 30 Lakini Musa alimwambia Yahweh, “Mimi sio mzuri wa kuongea, hivyo kwanini Farao anisikilize mimi?”