Waamuzi
1
1 Baada ya kifo cha Yoshua, wana wa Israeli walimuuliza Yahweh wakisema, “Ni nani atawashambulia kwanza Wakanaani kwa ajili yetu, ili kupigana nao? 2 Yahweh akasema, “Yuda atawashambulia. Tazama, nimewapa kumiliki nchi hii. 3 Watu wa Yuda wakawaambia wana wa Simeoni, ndugu zao, “Njoo pamoja nasi katika eneo letu ambalo tumepewa ili kwa pamoja tupigane na Wakanaani. Na sisi pia tutakwenda nanyi katika eneo mlilopewa.” Basi kabila la Simeoni wakaenda pamoja nao. 4 Watu wa Yuda wakashinda, na Bwana akawapa ushindi juu ya Wakanaani na Waperizi. Wakawaua watu elfu kumi huko Bezeki. 5 Wakamkuta Adoni Bezeki huko Bezeki, nao wakapigana naye na kuwashinda Wakanaani na Waperizi. 6 Lakini Adoni Bezeki akamkimbilia, wakamfuata na kumshika, nao wakavikata vidole gumba na vidole vyake vikubwa. 7 Adoni Bezek akasema, “Wafalme sabini, ambao na vidole gumba vyako na vidole vikubwa vilivyokatwa, walikusanya chakula chao chini ya meza yangu. Kama nilivyofanya, hata hivyo Mungu amefanya kwangu.” Wakamleta Yerusalemu, naye akafa huko. 8 Watu wa Yuda wakapigana dhidi ya jiji la Yerusalemu na kulichukua. Walishambulia kwa makali ya upanga na wakauwasha mji kwa moto. 9 Baada ya hayo, watu wa Yuda walikwenda kupigana na Wakanaani waliokaa mlimani, Negebu, na magharibi mwa milima. 10 Yuda akaenda dhidi ya Wakanaani waliokaa Hebroni (jina la Hebroni hapo awali ilikuwa Kiriath-arba), nao wakamshinda Sheshai, Ahimani na Talmai. 11 Kutoka huko watu wa Yuda walipigana na wenyeji wa Debiri (jina la Debiri hapo awali ilikuwa Kiriath-seferi). 12 Kalebu akasema, Yeyote atakayeivamia Kiriath-seferi na kuichukua, nitampa Aksa, binti yangu, awe mkewe. 13 Otinieli, mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu, akaiteka Debiri, naye Kalebu akampa Aksa, binti yake, awe mkewe. 14 Ndipo Aksa alifika kwa Othnieli, naye akamsihi amuombe baba yake ampe shamba. Alipokuwa akishuka katika punda wake, Kalebu akamwuliza, “Nikufanyie nini?” 15 Akamwambia, Nibariki. Kwa kuwa umenipa nchi ya Negebu, nipe pia chemchemi za maji. Kwa hiyo Kalebu akampa chemchemi za juu na chemchemi za chini. 16 Kizazi cha Mkeeni shemeji yake na Musa, walikwenda kutoka mji wa Mitende pamoja na watu wa Yuda, mpaka jangwa la Yuda, ambalo liko Negevu, kuishi na watu wa Yuda karibu na Arad. 17 Nao watu wa Yuda wakaenda pamoja na wana wa Simeoni ndugu zao, wakawaangamiza Wakanaani waliokaa Zefathi, wakaiharibu kabisa. Mji uliitwa Horma. 18 Watu wa Yuda pia waliiteka Gaza na nchi iliyoizunguka, Ashkeloni na nchi iliyoizunguka, na Ekron na nchi iliyoizunguka. 19 Yahweh alikuwa pamoja na watu wa Yuda na wakaimiliki nchi ya milima, lakini hawakuweza kuwatoa wenyeji wa kwenye bonde kwa sababu walikuwa na magari ya chuma. 20 Hebroni alipewa Kalebu (kama Musa alivyosema), naye akawafukuza kutoka huko wana watatu wa Anaki. 21 Lakini wana wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokaa Yerusalemu. Basi Wayebusi wakakaa na watu wa Benyamini huko Yerusalemu hata leo. 22 Nyumba ya Yusufu ilijiandaa kuishambulia Betheli, na Yahweh alikuwa pamoja nao. 23 Walipeleka watu kuipeleleza Betheli (jiji lililoitwa Luzu). 24 Wapelelezi waliona mtu akitoka nje ya jiji, wakamwambia, “Tafadhali tuonyeshe jinsi ya kuingia ndani ya jiji, na tutakutendea mema.” 25 Aliwaonyesha njia ya kuingia kwenye mji. Waliuteka mji kwa makali ya upanga, lakini wakamuacha mtu huyo na ndugu zake wote waondoke. 26 Na mtu huyo akaenda nchi ya Wahiti, akajenga mji, akauita Luzu, ambalo jina lake hata leo. 27 Watu wa Manase hawakuwafukuza watu waliokuwa katika miji ya Bethsheani na vijiji vyake, au Taanaki na vijiji vyake, au wale waliokaa Dori na vijiji vyake, wala wale waliokaa Ibleamu na vijiji vyake, wala walioshi Megido na vijiji vyake, kwa sababu Wakanaani walikuwa wameamua kuishi katika nchi hiyo. 28 Israeli ipokuwa na nguvu, waliwalazimisha Wakanaani wawatumikie kwa kazi ngumu, lakini hawakuwafukuza kabisa. 29 Efraimu hakuwafukuza Wakanaani waliokaa Gezeri; kwa hiyo Wakanaani wakakaa kati yao. 30 Zebuloni hakuwafukuza watu wa Kitroni, wala watu waliokuwa Nahaloli; na Wakanaani wakaendelea kuishi pamoja nao; lakini Zabuloni akawalazimisha Wakanaani wawatumikie kwa kazi ngumu. 31 Asheri hakuwafukuza watu wanaoishi Aka, au watu wanaoishi Sidoni, au wale wanaoishi Alabu, Akzib, Helba, Afeka, au Rehobu. 32 Kwa hiyo kabila ya Asheri iliishi kati ya Wakanaani (waliokaa katika nchi hiyo), kwa sababu hawakuwafukuza. 33 Na kabila la Naftali halikuwafukuza watu waliokuwa wakiishi Bethshemeshi, wala waliokuwa wakiishi Bethanathi. Kwa hiyo kabila la Naftali liliishi kati ya Wakanaani (watu waliokuwa wakiishi katika nchi hiyo). Hata hivyo, wenyeji wa Bethshemeshi na Bethanathi walilazimishwa kufanya kazi ngumu kwa Naphthali. 34 Waamori waliwalazimisha kabila la Dani kuishi katika nchi ya kilima, hawakuwaruhusu kuja bondeni. 35 Basi Waamori waliishi katika mlima wa Heresi, huko Aiyaloni, na Shaalbimu, lakini nguvu za kijeshi za nyumba ya Yusufu ziliwashinda, nao wakalazimishwa kuwatumikia kwa kazi ngumu. 36 Mpaka wa Waamori ulikuwa kutoka kilima cha Akrabimu huko Sela hadi nchi ya vilima.