17
“Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma yenye ncha ya almasi. Imechongwa kwenye kibao cha mioyo yao na kwenye pembe za madhabahu zako. Watoto wao wanakumbuka madhabahu zao na miti yao ya Ashera kwa miti ya majani kwenye milima mirefu. Mlima wangu katika nchi ya wazi na mali yako yote pamoja na hazina zako zote, nitakupa kama nyara kwa wengine. Hiyo ndiyo thamani ya maeneo yako ya juu na dhambi iliyo katika maeneo yako yote. Utapoteza urithi niliokupa. Nitakutumikisha kwa adui zako katika nchi ambayo hujui, kwa maana umewasha moto katika ghadhabu yangu, ambao utakawaka milele.” Bwana asema, “Mtu anayemtegemea mwanadamu amelaaniwa; amfanyaye mwanadamu kuwa nguvu yake na kugeuza moyo wake mbali na Bwana. Kwa maana atakuwa kama msitu mdogo katika Araba na hawezi kuona kitu kizuri kikija. Atakaa katika maeneo ya mawe jangwani, nchi isiyokuwa na wakazi. Lakini mtu anayemtegemea Bwana amebarikiwa, kwa kuwa Bwana ndiye tumaini lake. Kwa maana atakuwa kama mmea karibu na maji kando ya mto; mizizi yake itaenea. Hawezi kuona joto likija, kwa kuwa majani yake yatakuwa mabichi. Kisha mwaka wa ukame hawezi kuwa na wasiwasi, wala hataacha kuzalisha matunda. Moyo ni mdanganyifu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Una mgonjwa; ni nani anayeweza kuelewa? 10 Mimi ni Bwana, ninayechunguza akili, ambaye hujaribu viuno. Ninampa kila mtu kulingana na njia zake, kulingana na matunda ya matendo yake. 11 kama Kware akusanyaye mayai asiyotaga. Mtu anaweza kuwa tajiri kwa udhalimu, lakini wakati nusu ya siku zake ukipita, utajiri huo utamuacha, na mwishowe atakuwa mpumbavu.” 12 “Mahali pa hekalu letu ni kiti cha enzi cha utukufu, kilichoinuliwa tangu mwanzo. 13 Bwana ni tumaini la Israeli. Wote ambao wanakuacha watakuwa na aibu. Wale walio katika nchi ambao wanageuka kutoka kwako watauliwa. Kwa maana wamwacha Bwana, chemchemi ya maji yaliyo hai. 14 Niponye, Bwana, na mimi nitaponywa! Niokoe mimi, nami nitaokolewa. Kwa maana wewe ndio wimbo wangu wa sifa. 15 Tazama, wananiambia, 'Neno la Bwana liko wapi? Hebu lije!' 16 Mimi sikuwahi kuacha kuwa mchungaji nyuma yako. Sikuitamani siku ya maafa. Unajua yaliyotoka mdomoni mwangu. Yalifanyika mbele ya uwepo wako. 17 Usiwe sababu ya hofu kwangu. Wewe ni kimbilio langu siku ya msiba. 18 Waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi. Wataogopa, lakini usiache nifadhaike. Tuma siku ya maafa dhidi yao na kuwaangamiza maradufu.” 19 Bwana akaniambia hivi,: “Nenda ukasimame katika lango la watu ambako wafalme wa Yuda wanaingia na kutoka, basi katika malango mengine yote ya Yerusalemu. 20 Uwaambie, 'Sikieni neno la Bwana, wafalme wa Yuda, na ninyi watu wote wa Yuda, na kila mtu wa Yerusalemu atakayeingia kwa njia ya malango haya. 21 Bwana asema hivi: “Jihadharini kwa ajili ya maisha yenu na msichukue mzigo siku ya sabato ili muilete katika malango ya Yerusalemu. 22 Wala msilete mzigo nje ya nyumba zenu siku ya sabato. Msifanye kazi yoyote, lakini muitenge siku ya Sabato, kama nilivyowaagiza wazee wako kufanya.'” 23 Hawakusikiliza wala kutaega masikio yao, lakini walifanya shingo zao kuwa ngumu ili wasinisikilize wala kukubali maonyo. 24 Itatokea kwamba ikiwa mtanisikiliza kweli-hili ndilo tamko la Bwana-na msilete mzigo kwenye malango ya jiji hili siku ya sabato lakini badala yake mkatenga siku ya sabato kwa Bwana na msifanye kazi yoyote juu yake - 25 basi wafalme, wakuu, na wale wanaokaa kiti cha Daudi wataingia malango ya mji huu kwa magari na farasi, wao na viongozi wao, watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu. Na mji huu utakaa milele. 26 Watakuja kutoka miji ya Yuda na kutoka pande zote za Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini na visiwa vya chini, kutoka milimani na kutoka kaskazini, wakileta sadaka za kuteketezwa, dhabihu, sadaka za nafaka na ubani, sadaka za shukrani kwenye nyumba ya Bwana. 27 Lakini ikiwa hamtasikiliza-kutakasa siku ya Sabato, kutochukua mizigo nzito, wala msiingie milango ya Yerusalemu siku ya sabato, nitawasha moto katika malango yake, nao utaangamiza majumba kuteketeza ngome za Yerusalemu, na hauwezi kuzimika.