24
1 Kwa nini nyakati za kuwahukumu waovu hazikuwekwa na Mwenyezi? Kwa nini siyo wale waliowaaminifu kwa Mungu huziona siku za hukumu zikija? 2 Kuna waovu waondoao alama za mipaka; kuna waovu walichukua kundi kwa nguvu na kulifanya lao. 3 Wanawadhurumu wanyonge punda wao; wanachukua ng'ombe wa mjane kuwa dhamana. 4 Wanawaondoa wahitaji katika njia zao kwa lazima; masikini wa dunia yote wanajificha kutoka kwao. 5 Tazama, masikini hawa huenda kufanya kazi kama punda-mwitu mwituni, akitafuta chakula kwa uangalifu; pengine Araba itawapatia chakula kwa ajili ya watoto wao. 6 Masikini huvuna katika mashamba ya wengine usiku; wanakusanya zabibu kidogo kutokana na mapato ya waovu. 7 Wana lala bila kujifunika wakati wa usiku; hawana cha kujifunika wakati wa baridi. 8 Wanalowanishwa na mvua ya milimani; wanalala pembeni mwa miamba mikubwa kwani hawana makao. 9 Kuna waovu wanaowapokonya yatima katika kifua cha mama zao, na waovu wawachukuao watoto kama dhamana kutoka kwa masikini. 10 Lakini masikini wanatembea uchi; wajapokaa na njaa, wanabebea wengine chakula. 11 Masikini wanazalisha vinono ndani ya nyumba za waovu; wanakanyaga mashinikizo ya waovu, lakini wanakiu. 12 Watu wananung'unika mjini; waliojeruhiwa wanaomboleza, lakini Mungu hasikilizi maombi yao. 13 Baadhi ya waovu hawa wanaiasi nuru; hawafahamu njia zake, wala kukaa katika njia zake. 14 Muaji huinuka na nuru; huuwa masikini na waitaji; ni kama mwizi wakati wa usiku. 15 Pia, mzinifu hungoja wakati wa usiku; husema, 'Hakuna anionaye.' Hujibadilisha. 16 Waovu huingia katika nyumba gizani, lakini hujifungia wakati wa mchana; hawajari nuru. 17 Kwa kuwa asubuhi kwao wote ni kama giza totoro; wanaamani na vitisho vya giza totoro. 18 Wanapotea polepole, lakini, kama povu juu ya maji; shamba lao limelaaniwa; hakuna anayekwenda kufanya kazi katika mashamba yao ya mizabibu. 19 Kiangazi na joto huondoa barafu; ndivyo kuzimu pia kunavyowaaribu waliotenda dhambi. 20 Mama yake atamsahau; polepole funza watamuuma; hatakumbukwa tena; kwa hiyo, waovu watavunjika kama mti. 21 Mwovu anamrarua mgumba; hawatendi jema lolote kwa mjane. 22 Bado Mungu huwaondoa wenye nguvu kwa nguvu zake; huinuka na kuwadhoofisha. 23 Mungu huwaacha wajione wako salama, na wanalifurahia hilo, lakini anayaangalia maisha yao. 24 Watu hawa wanatukuzwa; bado, kitambo tu, watapotea; hakika, watashushwa; watakusanywa kama wengine wote; wataondolewa kama sehemu ya juu ya masikio ya nafaka. 25 Ikiwa sivyo, nani atanithibitisha kuwa mwongo; atakaye fanya maneno yangu kuwa si kitu?”