28
1 Hakika kuna machimbo ya fedha, wanaposafisha dhahabu. 2 Chuma uchimbwa; shaba uyeyushwa kutoka katika jiwe. 3 Mtu anaondoa giza na kutafuta, katika mpaka wa mbali, mawe hayaonekani na giza totoro. 4 Huchimba shimo mbali na makazi ya watu, mahali pasipopitwa na mtu. Huning'inia mbali na watu; uharakisha kwenda na kurudi. 5 Kwa nchi, kizalishwapo chakula, inapinduliwa kama kwa moto. 6 Mawe yake yana johari, na vumbi lake lina dhahabu. 7 Hata ndege mwindaji hapajui, wala jicho la kipanga halijapaona. 8 Ndege mwenye majivuna hajawai kuiona njia hiyo, wala simba mkali kupita pale. 9 Mtu huchimba mwamba mgumu; hupindua milima katika vyanzo vyake. 10 Huweka njia katika miamba; macho yake pale kila kilicho cha thamani. 11 Hufunga vyanzo hata wasiondoke; kilichofichika pale hukifunua. 12 Hekima itakuwa wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi? 13 Mtu hafahamu thamani yake; wala haipatikani katika nchi ya walio hai. 14 Vilindi vya maji chini ya nchi husema, 'Haiko kwangu'; bahari husema, 'Haipo pamoja nami.' 15 Hainunuliwi kwa dhahabu; wala hailinganishwi na fedha. 16 Haiwezi kuthamanishwa na dhahabu ya Ofiri, kwa jiwe jeusi la thamani au johari. 17 Dhahabu na fuwele hailingani nayo kwa thamani; wala haiwezi kubadilishwa kwa vito vya dhahabu safi. 18 Hailinganishwi na marijani wala yaspi; hakika, thamani ya hekima inapita madini ya rubi. 19 Topazi ya Ethiopia hailinganishwi nayo; wala kuthamanishwa kwa dhahabu safi. 20 Je hekima inatoka wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi? 21 Hekima imejificha mbali na macho ya viumbe wote na ndege wa angani. 22 Mauti na uharibifu husema, 'Tumesikia tu tetesi kwa masikio yetu.' 23 Mungu hufahamu njia ya kuipata; anapafahamu ilipo. 24 Kwani uona miisho yote ya dunia na huona chini ya mbingu zote. 25 Hapo kale, alifanya nguvu za upepo na kuyagawanya maji kwa kipimo. 26 Aliiwekea mvua tamko na njia ya radi na munguromo. 27 Kisha akaiona hekima na kuitangaza; aliianzisha, bila shaka, na kuipima. 28 Aliwambia watu, 'Tazameni, kumcha Bwana - ni hekima; kuacha uovu ni ufahamu.”