12
1 Wakati huo Yesu alienda siku ya sabato kupitia mashambani. Wanafunzi wake walikuwa na njaa na wakaanza kuyavunja masuke na kuyala. 2 Lakini Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu “Angalia wanafunzi wako wanavunja sheria wanatenda siku yasiyo yuhusiwa siku ya Sabato'' 3 Lakini Yesu akawaambia, “Hamjasoma jinsi Daudi aliyoyafanya, wakati alipokuwa na njaa, pamoja na watu aliokuwa nao? 4 Namna alivyoingia ndani ya nyumba ya Mungu na kula mikate ya wonyesho, ambayo ilikuwa siyo halali kwake kuila na wale aliokuwa nao, ila halali kwa Makuhani? 5 Bado hamjasoma katika sheria, kwamba katika siku ya Sabato Makuhani ndani ya hekalu huinajisi Sabato, lakini hawana hatia? 6 Lakini nasema kwenu kuwa aliye mkuu kuliko hekalu yuko hapa. 7 Kama mngalijua hii ina maanisha nini; nataka rehema na siyo dhabihu; msingaliwahukumu wasio na hatia, 8 Kwa kuwa Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” 9 Kisha Yesu akatoka pale akaenda katika sinagogi lao. 10 Tazama kulikuwa na mtu aliyepooza mkono. Mafarisayo wakamuuliza Yesu, wakisema. “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?” ili kwamba waweze kumshitaki kwa kutenda dhambi. 11 Yesu akawaambia, “Nani kati yenu, ambaye ikiwa ana kondoo mmoja, na huyu kondoo akaanguka ndani ya shimo siku ya sabato, hatamshika na kumtoa kwa nguvu ndani ya shimo? 12 Je, ni kipi chenye thamani, zaidi kwani, si zaidi ya kondoo! Kwa hivyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.'' 13 Kisha Yesu akamwambia yule mtu,” Nyoosha mkono wako” Akaunyoosha, na ukapata afya, kama ule mwingine. 14 Lakini Mafarisayo wakatoka njena wakapanga jinsi ya kumwangamiza walienda nje kupanga kinyume chake. Walikuwa wakitafuta jinsi ya kumuua. 15 Yesu alipoelewa hili aliondoka hapo. Watu wengi walimfuata, na akawaaponya wote. 16 Aliwaagiza wasije wakamfanya afahamike kwa wengine, 17 kwamba itimie ile kweli, iliyokuwa imesemwa na nabii Isaya, akisema, 18 Tazama, mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, katika yeye nafsi yangu imependezwa. Nitaweka Roho yangu juu yake, na atatangaza hukumu kwa Mataifa. 19 Hatahangaika wala kulia kwa nguvu; wala awaye yote kusikia sauti yake mitaani. 20 Hatalivunja tete lililochubuliwa; hatazima utambi wowote utoao moshi, mpaka atakapoleta hukumu ikashinda. 21 Na Mataifa watakuwa na ujasiri katika jina lake. 22 Mtu fulani kipofu na bubu, aliyepagawa na pepo aliletwa mbele ya Yesu. Akamponya, pamoja na matokeo ya kwamba mtu bubu alisema na kuona. 23 Makutano wote walishangaa na kusema,”Yaweza mtu huyu kuwa mwana wa Daudi?” 24 Lakini pindi Mafarisayo waliposikia muujiza huu, walisema, “Huyu mtu hatoi pepo kwa nguvu zake mwenyewe isipokuwa kwa nguvu za Belzebuli, mkuu wa pepo. 25 “Lakini Yesu alifahamu fikra zao na kuwaambia, “Kila ufalme uliogawanyika wenyewe huharibika, na kila mji au nyumba inayogawanyika yenyewe haitasimama. 26 Ikiwa Shetani, atamwondoa Shetani, basi anajipinga katika nafsi yake mwenyewe. 27 Ni namna gani ufalme wake utasimama? Na kama natoa pepo kwa nguvu za Belizabuli, wafuasi wenu huwatatoa kwa nija ya nani? Kwa ajili ya hili watakuwa mahakimu wenu. 28 Na kama natoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekjua kwenu. 29 Na mtu atawezaje kuingia ndani ya nyumba ya mwenye nguvu na kuiba, bila kumfunga mwenye nguvu kwanza? Ndiyo atakapoiba mali yake kutoka ndani ya nyumba. 30 Yeyote asiye kuwa pamoja nami yuko kinyume changu, naye asiye kusanya pamoja nami huyo hutawanya. 31 Kwa hiyo nasema kwenu, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, ila kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa. 32 Na yeyote asemaye neno kinyume cha Mwana wa Adamu, hilo atasamehewa. Lakini yeyote asemaye kinyume na Roho Mtakatifu, huyo hatasamehewa, katika ulimwengu huu, na wala ule ujao 33 Ama ufanye mti kuwa mzuri na tunda lake zuri, au uuharibu mti na tunda lake, kwa kuwa mti hutambulika kwa tunda lake. 34 Nyinyi kizazi cha nyoka, nyie ni waovu, mnawezaje kusema mambo mazuri? Kwa kuwa kinywa hunena kutoka katika akiba ya yaliyomo moyoni. 35 Mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoka mema, na mtu mwovu katika akiba ovu ya moyo wake, hutoa kilicho kiovu. 36 Nawaambia kuwa katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu ya kila neno lisilo na maana walilosema. 37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa.” 38 Kisha baadhi ya waandishi na Mafarisayo walimjibu Yesu wakisema” Mwalimu, tungependa kuona ishara kutoka kwako.” 39 Lakini Yesu alijibu na kuwaambia, “Kizazi kiovu na cha zinaa kinatafuta ishara. Lakini hakuna ishara itakayotolewa kwao isipokuwa ile ishara ya Yona nabii. 40 Kama vile nabii Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu mchana na usiku, hivyo ndivyo Mwana wa Adam atakavyo kuwa ndani ya moyo wa nchi kwa siku tatu mchana na usiku. 41 Watu wa Ninawi watasimama mbele ya hukumu pamoja na kizazi cha watu hawa na watakihukumu. Kwa kuwa walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, mtu fulani mkuu kuliko Yona yuko hapa. 42 Malkia wa kusini atainuka kwenye hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki na kukihukumu. Alikuja toka miisho ya dunia kuja kusikia hekima ya Selemani, na tazama, mtu fulani mkuu kuliko Selemani yupo hapa. 43 Wakati pepo mchafu amtokapo mtu, hupita mahali pasipo na maji akitafuta kupumzika, lakini hapaoni 44 Kisha husema, 'nitarudi kwenye nyumba yangu niliyotoka.' Arudipo hukuta ile nyumba imesafishwa na iko tayari. 45 Kisha huenda na kuwaleta wengine roho wachafu saba walio wabaya zaidi kuliko yeye, huja kuishi wote pale. Na hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Hivyo ndivyo itakavyo kuwa kwa kizazi hiki kiovu. 46 Wakati Yesu alipokuwa akizungumza na umati tazama, mama yake na ndugu zake walisimama nje, wakitafuta kuongea naye. 47 Mtu mmoja akamwambia, “Tazama mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanatafuta kuongea nawe”. 48 Lakini Yesu alijibu na kumwambia aliyemjulisha, “Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?” 49 Naye alinyoosha mkono wake kwa wanafunzi na kusema, “Tazama, hawa ni mama na ndugu zangu! 50 Kwa kuwa yeyote afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, mtu huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu”.