4
Lakini katika siku za mwisho itakuja kuhusu kwamba mlima wa nyumba ya Yahwe utawekwa imare juu ya milima mingine. Utainuliwa juu ya milima, na watu watautakabisha. Mataifa mengi yataenda na kusema, “Njoni, twendeni juu kwenye mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, na tutembea katika njia zake.” Kwa kuwa kutoka Sayuni sheria itatoka, na neno la Yahwe kutoka Yerusalemu. Atahukumu miongoni mwa watu na kuamua kuhusiana na mataifa mengi ya mbali. Watapoga mapanga yao kuwa plau na mikuki yao kuwa miuundu ya kupogolea. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa, wala kutawala kwa vita tena. Badala yake, wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake. Hakuna mtu atakayewafanya waogope, kwa kuwa mdomo wa Yahwe wa majeshi umesema. Kwa kuwa watu wote wataenenda, kila mmoja, katika jina la mungu wake. Lakini sisi tutaenenda katika jina la Yahwe Mungu wetu milele na milele. “Katika siku hiyo,” aseme Yahwe, “Nitamkusanya achechemeaye na kumkusanya aliyefukuzwa, wale ambao nimewatesa. Nitamrudisha aliyechechemea kwenye mabaki, na yeye aliyetupwa kwenye taifa imara, na mimi, Yahwe, nitatawala juu yao katika Milima Sayuni, sasa na milele. Kama kwako, mnara wa saa kwa ajili ya kundi, mlima wa binti wa Sayuni-utakuja kwenu, utawala wenu wa zamani utarudishwa, ufalme ambao unaomilikiwa na binti wa Yerusalemu. Sasa, kwa nini unapiga kelele kwa sauti kuu? Je hakuna mfalme miongoni mwenu? Je mshauri wako amekufa? Kwa nini uchungu umekushika kama yule mwanamke akiwa anazaa? 10 Kuwa katika uchungu wa kuzaa ili uzae, binti Sayuni, kama mwanamke mwenye uchungu. Kwa sasa utatoka nje ya mji, kuishi kwenye shamba, na kwenda Babeli. Huko utaokolewa. Huko Yahwe atakuokoa kutoka kwenye mikono ya maadui. 11 Sasa mataifa mengi yamekusanyika juu yako; wakisema; 'Atiwe unajisi; macho yenu yaangalie Sayuni.”' 12 Nabii asema, “Hawayajui mawazo ya Yahwe, wala hawaelewi mpango wake, kwa kuwa wamewakusanaya kama miganda kupura sakafuni.” 13 Yahwe asema, “siamama na upure, binti Sayuni, kwa kuwa nitaifanya pembe yako kuwa chuma, na nitazifanya kwato zako kuwa shaba. Utaponda watu wengi. Nitaweka wakfu udhalimu wao kwangu mwenyewe, Yahwe, miliki zao kwangu, Bwana wa dunia nzima.”