9
1 Na alisema kwao, “Hakika nasema kwenu, baadhi yenu kuna watu waliosimama hapa hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.” 2 Na baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana pamoja naye mlimani, pekee yao. Ndipo alianza kubadilika mbele yao. 3 Mavazi yake yakaanza kung'aa sana, meupe zaidi, meupe kuliko mng'arishaji yeyote duniani. 4 Ndipo Eliya pamoja na Musa walitokea mbele yao, na walikuwa wakiongea na Yesu. 5 Petro alijibu akamwambia Yesu, “Mwalimu, ni vyema sisi kuwa hapa, na tujenge vibanda vitatu, kimoja kwa ajili yako, kimoja kwa ajili Musa na kingine kwa ajili ya Eliya.” 6 (Kwa kuwa hakujua nini cha kusema, waliogopa sana.) 7 Wingu lilitokea na kuwafunika. Ndipo sauti ikatoka mawinguni ikisema, “ Huyu ni mwanangu mpendwa. Msikieni yeye.” 8 Ghafla, walipokuwa wakitazama, hawakumuona yeyote pamoja nao, isipokuwa Yesu tu. 9 Walipokuwa wanateremka kutoka mlimani, aliwaamuru kutokumwambia mtu yeyote yale yote waliyoyaona, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka kwa wafu. 10 Ndipo waliyatunza mambo wao wenyewe. Lakini walijadiliana wao kwa wao ni nini maana yake “kufufuliwa kutoka kwa wafu” 11 Walimwuliza Yesu,”Kwa nini waandishi husema lazima Eliya aje kwanza?” 12 Akawaambia, “hakika Eliya atakuja kwanza kuokoa vitu vyote. Kwa nini imeandikwa Mwana wa Adamu lazima apate mateso mengi na achukiwe? 13 Lakini nasema kwenu Eliya alikwisha kuja, na walimfanya kama walivyopenda, kama vile maandiko yasemavyo kuhusu yeye.” 14 Na waliporudi kwa wanafunzi, waliona kundi kubwa limewazunguka na Masadukayo walikuwa wanabishana nao. 15 Na mara walipomwona, kundi lote lilishangaa na kumkimbilia kumsalimia. 16 Aliwauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao juu ya nini?” 17 Mmoja wao katika kundi alimjibu, “Mwalimu, nilimleta mwanangu kwako; ana roho chafu ambayo humfanya asiweze kuongea, 18 na humsababishia kutetemeka na kumwangusha chini, na kutoka povu mdomoni na kusaga meno na kukakamaa. Niliwaomba wanafunzi wako kumtoa pepo, lakini hawakuweza. 19 Aliwajibu, “Kizazi kisichoamini, nitakaa nanyi kwa muda gani? Nitachukuliana nanyi hadi lini? Mleteni kwangu.” 20 Walimleta mtoto wake. Roho mchafu alipomwona Yesu, ghafla ilimtia katika kutetemeka. Mvulana alianguka chini na kutoa povu mdomoni. 21 Yesu alimwuliza baba yake, “Amekuwa katika hali hii kwa muda gani?” Baba alisema, “ Tangu utoto. 22 Mara nyingine huanguka katika moto au kwenye maji, na kujaribu kumwangamiza. Kama unaweza kufanya chochote tuhurumie na utusaidie.” 23 Yesu alimwambia, “Kama uko tayari? Kila kitu kinawezekana kwa yeyote aaminiye.” 24 Ghafla baba wa mtoto alilia na kusema, “ Naamini! Nisaidie kutokuamini kwangu.” 25 Wakati Yesu alipoona kundi linakimbilia kwao, alimkemea roho mchafu na kusema, “wewe roho bubu na kiziwi, nakuamuru mwache, usiingie kwake tena.” 26 Alilia kwa nguvu na kumhangaisha mtoto na roho alimtoka. Mtoto alionekana kama amekufa, Ndipo wengi walisema, “Amekufa,” 27 Lakini Yesu alimchukua kwa mkono akamwinua, na mtoto alisimama. 28 Wakati Yesu alipoingia ndani, wanafunzi wake walimwuliza faragha, “Kwa nini hatukuweza kumtoa?” 29 Aliwaambia, “ kwa namna hii hatoki isipokuwa kwa maombi.” 30 Walitoka pale na kupitia Galilaya. Hakutaka mtu yeyote ajue walipo, 31 kwa kuwa alikuwa anafundisha wanafunzi wake. Aliwaambia, “Mwana wa Adamu atafikishwa mikononi mwa watu, na watamuua. Atakapokuwa amekufa, baada ya siku tatu atafufuka tena.” 32 Lakini hawakuelewa maelezo haya, na waliogopa kumwuliza. 33 Ndipo walifika Karperinaumu. Wakati akiwa ndani ya nyumba aliwauliza, ''Mlikuwa mnajadili nini njiani”? 34 Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi. 35 Alikaa chini akawaita kumi na wawili pamoja, na alisema nao, “Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.” 36 Alimchukua mtoto mdogo akamweka katikati yao. Akamchukua katika mikono yake, akasema, 37 “Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma.” 38 Yohana alimwambia, “Mwalimu tulimwona mtu anatoa pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu hatufuati.” 39 Lakini Yesu alisema, “Msimzuie, kwa kuwa hakuna atakayefanya kazi kubwa kwa jina langu na ndipo baadaye aseme neno baya lolote juu yangu. 40 Yeyote asiyekuwa kinyume nasi yuko upande wetu. 41 Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu uko na Kristo, kweli nawaambia, hatapoteza thawabu yake. 42 Yeyote anayewakosesha hawa wadogo waniaminio mimi, ingekuwa vyema kwake kufungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutupwa baharini. 43 Kama mkono wako ukikukosesha ukate. Ni heri kuingia katika uzima bila mkono kuliko kuingia kwenye hukumu ukiwa na mikono yote. Katika moto “usiozimika”. 44 (Zingatia: Mstari hii, “Mahali ambapo funza hawafi na moto usiozimika.” haumo katika nakala za kale). 45 Kama mguu wako ukikukosesha, ukate. Ni vyema kwako kuingia uzimani ukiwa kilema, kuliko kutupwa hukumuni na miguu miwili. 46 (Zingatia: Mstari huu, “Mahali ambapo funza hawafi na moto usioweza kuzimika” haumo kwenye nakala za kale). 47 Kama jicho lako likikukosesha ling'oe. Ni vyema kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa kuzimu. 48 Mahali palipo na funza wasiokufa, na moto usiozimika. 49 Kwa kuwa kila mmoja atakolezwa na moto. 50 Chumvi ni nzuri, kama chumvi ikipoteza ladha yake, utaifanyaje iwe na ladha yake tena? Muwe na chumvi miongoni mwenu wenyewe, na muwe na amani kwa kila mmoja.”