12
Kisha Yesu alianza kuwafundisha kwa mifano. Akasema, “Mtu alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia uzio, na akachimba shimo la kusindika mvinyo. Akajenga mnara na kisha akalipangisha shamba la mizabibu kwa wakulima wa mizabibu. Kisha alisafiri safari ya mbali. Wakati ulipofika, alimtuma mtumishi kwa wakulima wa mizabibu kupokea kutoka kwao baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini walimkamata, wakampiga, na wakamfukuza bila chochote. Akamtuma kwao mtumishi mwingine, wakamjeruhi kichwani na kumtendea mambo ya aibu. Bado alimtuma mwingine, na huyu mmoja walimwua. Waliwatendea wengine wengi mambo kama hayo hayo, wakiwapiga na wengine kuwaua. Alikuwa bado na mtu mmoja zaidi wa kumtuma, mwana mpendwa. Naye alikuwa wa mwisho aliyetumwa kwao. Akisema, “Watamheshimu mwanangu”. Lakini wapangaji walisemezana wao kwa wao, “Huyu ndiye mrithi. Njoni, hebu na tumwue, na urithi utakuwa wetu.” Walimvamia, wakamuua na kumtupa nje ya shamba la mizabibu. Kwa hiyo, Je! Atafanya nini mmiliki wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wa mizabibu na atalikabidhi shamba la mizabibu kwa wengine. 10 Hamjapata kusoma andiko hili? “Jiwe ambalo wajenzi walilikataa, limekuwa jiwe la pembeni. 11 Hili lilitoka kwa Bwana, na ni la ajabu machoni petu.” 12 Walitafuta kumkamata Yesu, Lakini waliwaogopa makutano, kwani walijua kuwa alikuwa amenena mfano huo dhidi yao. Hivyo walimwacha na wakaenda zao. 13 Kisha wakawatuma baadhi ya mafarisayo na maherodia kwake ili kumtega kwa maneno. 14 Walipofika, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba hujali maoni ya yeyote na huonyeshi upendeleo kati ya watu. Unafundisha njia ya Mungu katika ukweli. Je! Ni haki kulipa kodi kwa Kaisari au la? Je! Twaweza kulipa au la? 15 Lakini Yesu alijua unafiki wao na kuwaambia, “Kwa nini mnanijaribu? Nipeni dinari niweze kuitazama.” 16 Wakaleta moja kwa Yesu, Akawaambia, “Je! ni sura ya nani na maandishi yaliyopo hapa ni ya nani? Wakasema, “Ya Kaisari.” 17 Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vya Kaisari na Mungu vitu vya Mungu.” Wakamstaajabia. 18 Kisha Masadukayo, wasemao hakuna ufufuo, walimwendea. Wakamuwuliza, wakisema, 19 “Mwalimu, Musa alituandikia kuwa, 'Ikiwa ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke nyuma yake, lakini hakuacha mtoto, mtu atamchukua mke wa ndugu yake, na kujipatia watoto kwa ajili ya ndugu yake.' 20 Kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza alitwaa mke na kisha akafa, hakuacha watoto. 21 Kisha wa pili alimchukua naye akafa, hakuacha watoto. Na wa tatu hali kadhalika. 22 Na wa saba alikufa bila kuacha watoto. Mwishowe na mwanamke pia akafa. 23 Wakati wa ufufuo, watakapofufuka tena, Je! Atakuwa mke wa nani? Kwani wale ndugu wote saba walikuwa waume wake.” 24 Yesu aliwaambia, “Je! Hii si sababu kuwa mmepotoshwa, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?” 25 Wakati wa kufufuka toka kwa wafu, hawataoa wala kuingia katika ndoa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni. 26 Lakini, kuhusu wafu ambao wanafufuliwa, Je! Hamkusoma kutoka katika kitabu cha Musa, katika habari za kichaka, jinsi Mungu alivyosema na kumwambia, 'Mimi ni Mungu wa Abrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?' 27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Ni dhahiri mmepotoka.” 28 Mmoja wa waandishi alikuja na kuyasikia mazungumzo yao; aliona kwamba Yesu aliwajibu vema. Alimwuliza, “Je! ni amri ipi iliyo ya muhimu zaidi katika zote?” 29 Yesu alimjibu, “Iliyo ya muhimu ni hii, “Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja. 30 Lazima umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako yote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote.' 31 Amri ya pili ni hii, 'Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.' Hakuna amri nyingine kuu zaidi ya hizi.” 32 Mwandishi akasema, “Vema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake. 33 Kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mwenyewe, ni muhimu mno kuliko matoleo na dhabihu za kuteketeza.” 34 Wakati Yesu alipoona ametoa jibu la busara, alimwambia, “Wewe hauko mbali na ufalme wa Mungu.” Baada ya hapo hakuna hata mmoja aliye thubutu kumwuliza Yesu maswali yoyote. 35 Na Yesu alijibu, wakati alipokuwa akifundisha katika hekalu, akasema, “Je! waandishi husemaje kuwa Kristo ni mwana wa Daudi? 36 Daudi mwenyewe katika Roho Mtakatifu, alisema, 'Bwana alisema kwa Bwana wangu, keti katika mkono wangu wa kuume, mpaka niwafanye maadui wako kuwa chini ya miguu yako.' 37 Daudi mwenyewe humwita Kristo, 'Bwana' Je! ni mwana wa Daudi kwa jinsi gani?” Na kusanyiko kuu lilimsikiliza kwa furaha. 38 Katika mafundisho yake Yesu alisema, “Jihadharini na waandishi, wanaotamani kutembea na kanzu ndefu na kusalimiwa kwenye masoko 39 na kuketi kwenye viti vya wakuu katika masinagogi na katika sikukuu kwa maeneo ya wakuu. 40 Pia wanakula nyumba za wajane na wanaomba maombi marefu ili watu wawaone. Hawa watu watapokea hukumu iliyo kuu.” 41 Kisha Yesu aliketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa. 42 Kisha mwanamke mjane maskini alikuja na kutia vipande viwili, thamani ya senti. 43 Kisha akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, “Amini nawaambia, mwanamke huyu mjane ametia kiasi kikubwa zaidi ya wote ambao wameshatoa katika sanduku la sadaka. 44 Kwani wote wametoa kutokana na wingi wa mapato yao. Lakini mwanamke mjane huyu, kutoka katika umaskini wake, katia pesa yote ambayo alipaswa kuitumia kwa maisha yake.”