10
Wale ambao waliweka majina yao kwenye nyaraka zilizofunikwa walikuwa Nehemia mwana wa Hakalia gavana, na makuhani waliowekwa walikuwa Sedekia, Seraya, Azaria, Yeremia, Pashuri, Amaria, Malkiya, Hamshi, Shekania, Maluki, Harimu, Meremothi, Obadia, Danieli, Ginethoni, Baruki, Meshulamu, Abiya, Miyamini, Maazia, Bilgai na Shemaya. Hawa walikuwa makuhani. Walawi walikuwa Yeshua mwana wa Azania, Binui wa jamaa ya Henadadi, Kadmieli, 10 na Walawi wenzake, Shebania, Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani, 11 Mika, Rehobu, Hashabia, 12 Zakuri, Sherebia, Shebania, 13 Hodiya, Bani na Beninu. 14 Viongozi wa watu walikuwa Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani, 15 Buni, Azgadi, Bebai, 16 Adoniya, Bigwai, Adini, 17 Ateri, Hezekia, Azuri, 18 Hodia, Hashumu, Besai, 19 Harifu, Anathothi, Nobai, 20 Magpiashi, Meshulamu, Heziri, 21 Meshezabeli, Sadoki, Yadua, 22 Pelatia, Hanani, AnaYA, 23 Hoshea, Hanania, Hashubu, 24 Haloheshi, Pilha, Shobeki, 25 Rehumu, Hashabna, Maaseya, 26 Ahia, Hanani, Anani, 27 Maluki, Harimu na Baana. 28 Na watu wengine waliokuwa makuhani, na Walawi, na walinzi wa malango, na waimbaji, na watumishi wa hekalu, na wote waliokuwa wamejitenga wenyewe na watu wa nchi za jirani, kwa sheria ya Mungu, na wanawake zao, na wana wao, na Binti zao, wote walio na ujuzi na ufahamu, 29 walijiunga na ndugu zao, wakuu wao, na kujifunga katika laana na kiapo cha kutembea katika sheria ya Mungu, iliyotolewa na Musa mtumishi wa Mungu, na kuzingatia na kutii amri zote za Bwana Mungu wetu na hukumu zake na sheria zake. 30 Tuliahidi kuwa hatuwezi kuwapa binti zetu watu wa nchi au kuchukua binti zao kwa wana wetu. 31 Pia tuliahidi kwamba ikiwa watu wa nchi wataleta bidhaa au nafaka yoyote ya kuuza siku ya Sabato, hatuwezi kununua kutoka kwao siku ya Sabato au siku yoyote takatifu. Kila mwaka wa saba tutaacha mashamba yetu kupumzika, na tutafuta madeni yote yaliyotokana na Wayahudi wengine. 32 Tulikubali amri za kutoa shilingi ya shekeli kila mwaka kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu wetu, 33 kutoa mkate wa uwepo, na sadaka ya nafaka ya kawaida, sadaka za kuteketezwa siku za Sabato, sikukuu mpya za mwezi na sikukuu za kuteketezwa, na sadaka takatifu, na sadaka za dhambi za kufanya upatanisho kwa Israeli, pamoja na kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu. 34 Na makuhani, Walawi, na watu wakapiga kura kwa ajili ya sadaka ya kuni. Kura ilichagua ni nani wa familia zetu ataleta kuni ndani ya nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati zilizowekwa kila mwaka. Kuni hizo zilichomwa juu ya madhabahu ya Bwana Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika sheria. 35 Tuliahidi kuleta nyumbani kwa Bwana matunda ya kwanza yaliyotokana na udongo wetu, na matunda ya kwanza ya mti kila mwaka. 36 Na kama ilivyoandikwa katika sheria, tuliahidi kuleta nyumbani kwa Mungu na kwa makuhani watumikao hapo wazaliwa wa kwanza wa wana wetu ma wanyama wetu. 37 Tutaleta unga wa kwanza na sadaka zetu za nafaka, na matunda ya kila mti, na divai mpya na mafuta tutaleta kwa makuhani, kwenye vyumba vya kuhifadhi vya nyumba ya Mungu wetu. Tutawaletea Walawi sehemu ya kumi kutoka kwenye udongo wetu kwa sababu Walawi hukusanya zaka katika miji yote tunayofanya kazi. 38 Kuhani, mzao wa Haruni, lazima awe na Walawi wakati wanapopokea zaka. Walawi wanapaswa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu kwenye vyumba vya kuhifadhi hazima. 39 Kwa maana wana wa Israeli na wana wa Lawi, wataleta sadaka za nafaka, divai mpya, na mafuta katika vyumba vya kuhifadhi ambapo vitu vya patakatifu vinasimamishwa, na mahali pa makuhani watumishi, na walinzi wa mlango, na waimbaji. Hatuwezi kuacha nyumba ya Mungu wetu.