10
1 Kwa vile sheria ni kivuli cha mambo mema yajayo, si yale yaliyo halisi. Sheria kamwe haiwezi kuwakamilisha wale ambao wanaomkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu zilezile ambazo makuhani waliendelea kutoa mwaka baada ya mwaka. 2 Au vinginevyo dhabihu hizo zisingeweza kukoma kutolewa? Kwa kigezo hicho waabuduo, wakiwa wamesafishwa mara moja, wasingelikuwa na utambuzi zaidi wa dhambi. 3 Bali katika dhabihu hizo kuna ukumbusho wa dhambi zilizotendwa mwaka baada ya mwaka. 4 Kwa kuwa haiwezekani kwa damu ya mafahari na mbuzi kuziondoa dhambi. 5 Wakati Kristo alipokuja duniani, alisema, “Hamkutamani matoleo au dhabihu, badala yake, mliandaa mwili kwa ajili yangu. 6 Hamkuwa na thamani katika matoleo yote ya kuteketezwa au dhabihu kwa ajili ya dhambi. 7 Kisha nilisema, “Ona, hapa ninayafanya mapenzi yako, Mungu, kama ilivyoandikwa kunihusu mimi katika gombo”. 8 Alisema kama ilivyo semwa hapo juu: “Hamkutamani dhabihu, matoleo, au sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi, wala hukuona furaha ndani yake” dhabihu ambazo zinatolewa kulingana na sheria. 9 Kisha alisema, “Ona, niko hapa kufanya mapenzi yako”. Ameweka pembeni taratibu zilizo za awali ili kuimarisha zile za pili. 10 Katika taratibu za pili, tumekwisha tengwa kwa Mungu kwa mapenzi yake kupitia kujitoa kwa mwili wa Yesu Kristo mara moja kwa nyakati zote. 11 Ni kweli, kila kuhani husimama kwa huduma siku kwa siku, akitoa dhabihu ile ile, ambayo, kwa vyovyote, kamwe isingeweza kuziondoa dhambi. 12 Lakini baada ya Kristo kutoa dhabihu mara moja kwa dhambi milele yote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu, 13 akisubiri mpaka maadui zake watiwe chini na kufanywa kiti kwa ajili ya miguu yake. 14 Kwa kuwa kwa njia ya toleo moja amewakamilisha milele wale ambao wametengwa kwa Mungu. 15 Na Roho Mtakatifu pia ashuhudia kwetu. Kwa kuwa kwanza alisema, 16 “Hili ni agano nitakalofanya pamoja nao baada ya siku hizo; asema Bwana: nitaweka sheria zangu ndani ya mioyo yao, na nitaziandika katika akili zao”. 17 Kisha alisema, “Hawatazikumbuka tena dhambi na matendo yao mafu”. 18 Sasa mahali palipo na msamaha kwa hawa, hakuna tena dhabihu yoyote kwa ajili ya dhambi. 19 Kwa hiyo, ndugu, tunao ujasiri wa kuingia mahali patakatifu zaidi kwa damu ya Yesu. 20 Hiyo ni njia ambayo ameifungua kwa ajili yetu kwa njia ya mwili wake, mpya na hai inayopitia kwenye pazia. 21 Na kwa sababu tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu, 22 na tumkaribie na moyo wa kweli katika utimilifu wa uhakika wa imani tukiwa na mioyo iliyonyunyiziwa safi kutoka uovu wa dhamiri na kuwa na miili yetu iliyooshwa kwa maji safi. 23 Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu. 24 Na tuzidi kutafakari namna ya kumtia moyo kila mmoja kupenda na matendo mema. 25 Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia. 26 Kama tukifanya makusudi kuendelea kutenda dhambi baada ya kuwa tumepokea elimu ya ukweli, Dhabihu nyingine ya dhambi haisalii tena. 27 Badala yake, kuna tarajio pekee la hukumu ya kutisha, na ukali wa moto ambao utawateketeza maadui wa Mungu. 28 Yeyote ambaye ameikataa sheria ya Musa hufa bila rehema mbele ya ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu. 29 kiwango gani zaidi cha adhabu unafikiri kinamstahiri kilammoja ambaye amemdharau mwana wa Mungu, yeyote aliyeitendea damu ya agano kama kitu kisicho kitakatifu, damu ambayo kwayo aliiweka wakfu kwa Mungu - yeyote ambaye amemtukana Roho wa neema? 30 Kwakuwa tunajua mmoja ambaye aliyesema, “Kisasi ni changu, nitalipa”. Na tena, “Bwana atawahukumu watu wake”. 31 Ni jambo la kuogofya mtu kuangukia katika mikono ya Mungu aliye hai! 32 Lakini kumbuka siku zilizopita, baada ya kutiwa kwenu nuru, ni jinsi gani mliweza kuvumilia maumivu makali. 33 Mlikuwa mmewekwa wazi katika dhihaka ya matukano na mateso, na mlikuwa washiriki pamoja na wale waliopitia mateso kama hayo. 34 Kwa kuwa mlikuwa na moyo wa huruma kwa hao waliokuwa wafungwa, na mlipokea kwa furaha adhabu ya urithi wenu, mkijua kwamba ninyi wenyewe mlikuwa na urithi bora na wa kudumu milele. 35 Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, ulio na zawadi kuu. 36 Kwa kuwa mnahitaji uvumilivu, ili kwamba mpate kupokea ambacho Mungu amekiahidi, baada ya kuwa mmekwisha yatenda mapenzi yake. 37 Kwa kuwa baada ya kitambo kidogo, mmoja anayekuja, atakuja hakika na hatakawia. 38 Mwenye haki wangu ataishi kwa imani. Kama atarudi nyuma, sitapendezwa naye.” 39 Lakini sisi si kama wale warudio nyuma kwa kuangamia. Badala yake, sisi ni baadhi ya wale tulio na imani ya kuzilinda roho zetu.