Zaburi. 3. Yahewh, maadui zangu wako wangapi! Ni wengi wamekuja kinyume na mimi. Ni wengi wanaonisema, “Hakuna msaada wowote kutoka kwa Mungu kwa ajili yake.” Selah Bali wewe, Yahweh, u ngao yangu pande zote, utukufu wangu, na uniinuaye kichwa changu. Nampazia Yahweh sauti yangu, na yeye ananijibu kutoka katika mlima wake mtakatifu. Nilijilaza chini na kusinzia; na niliamka, kwa kuwa Yahweh alinilinda. Sitaogopa kusanyiko la watu ambao wamejipanga kinyume na mimi pande zote. Inuka, Yahweh! Uniokoe, Mungu wangu! Kwa kuwa utawapiga maadui zangu wote kwenye taya zao; utayavunja meno ya waovu. Wokovu unatoka kwa Yahweh. Baraka zako ziwe juu ya watu wako.