Zaburi. 64. Sikia sauti yangu, Mungu, usikilize malalamiko yangu; unilinde dhidi ya hofu ya adui zangu. Unifiche dhidi ya mipango ya siri ya wafanyao maovu, unifiche dhidi ya watendao vurugu ya udhalimu. Wao wamenoa ndimi zao kama panga; wamelenga mishale yao, maneno machungu, ili kwamba waweze kupiga kutoka mahali pa siri kwenda kwa mtu asiye na hatia; wampige yeye kwa ghafla nao wasihofu lolote. Wao wanahamasishana wenyewe katika kupanga uovu; wanashauriana pamoja wao binafsi ili kuweka mitego; nao husema, “Ni nani atakayetuona?” Wanabuni mipango ya dhambi; “Tumemaliza,” wanasema, “ni mpango makini.” Mawazo ya ndani na mioyo ya watu ni ya kina. Lakini Mungu atawapiga wao; ghafla watajeruhiwa kwa mishale yake. Watafanywa kuwa mashakani, kwa kuwa ndimi zao wenyewe ziko kinyume nao; wote wawaonao watatikisa vichwa vyao. Watu wote wataogopa na kutangaza matendo ya Mungu. Kwa hekima watafikiria kuhusu kile yeye ametenda. Wenye haki watakuwa na furaha kuhusu Yahwe nao watakimbilia kwake; wote wenye haki moyoni watajivuna katika yeye.