Zaburi. 67. Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote. Watu wakusifu wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani. Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. Nchi imetoa mavuno yake na Mungu, Mungu wetu, ametubariki. Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.