7
1 Wakati ukuta ulipomalizika na milango nimekwisha kuisimamisha, na walinzi wa malango na waimbaji na Walawi walikuwa wamechaguliwa, 2 nikampa ndugu yangu Hanani kuwa na amri juu ya Yerusalemu, pamoja na Hanania ambaye alikuwa msimamizi wa kijiji, kwa kuwa alikuwa mwaminifu na alimuogopa Mungu zaidi kuliko wengi. 3 Nami nikawaambia, Msifungue malango ya Yerusalemu mpaka jua litakapokuwa kali. Wakati walinzi wa mlango wanalinda, unaweza kufunga milango na kuikaza. Chagua walinzi kutoka kwa wale wanaoishi Yerusalemu, wengine mahali pa kituo chao cha ulinzi, na wengine mbele ya nyumba zao wenyewe. 4 Sasa jiji lilikuwa pana na kubwa, lakini kulikuwa na watu wachache ndani yake, na hakuna nyumba zilizojengwa tena. 5 Mungu wangu aliweka moyoni mwangu, kuwakusanya pamoja wakuu, maafisa, na watu kuwaandikisha katika familia zao. Nilipata Kitabu cha kizazi cha wale ambao walirudi kwanza na nikaona kwamba imeandikwa humo. 6 Hawa ndio watu wa jimbo ambao walikwenda kutoka kwenye uhamisho wa wale waliohamishwa ambao Nebukadreza mfalme wa Babeli aliwachukua mateka. Wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenda kwenye mji wake. 7 Walikuja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana. Idadi ya wana wa Israeli ilikuwa. 8 Wana wa Paroshi, 2, 172. 9 Wana wa Shefatia, 372. 10 Wana wa Ara, 652. 11 Wana wa Pahath Moabu, 12 kwa wana wa Yeshua na Yoabu, 2, 818. 13 Wana wa Elamu, 1, 254. 14 Wana wa Zatu, 845. Wana wa Zakai, 760. 15 Wana wa Binnui, 648. 16 Wana wa Bebai, 628. 17 Wana wa Azgadi, 2, 322. 18 Wana wa Adonikamu, 667. 19 Wana wa Bigwai, 2, 067. 20 Wana wa Adini, 655. 21 Wana wa Ateri, wa Hezekia, 98. 22 Wana wa Hashumu, 328. 23 Wana wa Besai, 324. 24 Wana wa Harifu, 112. 25 Wana wa Gibeoni, 95. 26 Watu kutoka Bethlehemu na Netofa, 188. 27 Watu wa Anathothi, 128. 28 Watu wa Beth Azmaweth, 42. 29 Watu wa Kiriath Yearimu, Kefira, na Beerothi, 743. 30 Watu wa Rama na Geba, 621. 31 Watu wa Mikmasi, 122. 32 Watu wa Betheli na Ai, 123. 33 Watu wa Nebo, 52. 34 Watu wa Elamu wa pili, 1, 254. 35 Watu wa Harimu, 320. 36 Watu wa Yeriko, 345. 37 Watu wa Lodi, Hadidi, na Ono, 721. 38 Watu wa Senaa, 3, 930. 39 makuhani Wana wa Yedaya (wa nyumba ya Yeshua), 973. 40 Wana wa Imeri, 1, 052. 41 Wana wa Pashuri, 1, 247. 42 Wana wa Harimu, 1, 017. 43 Walawi, wana wa Yeshua, wa Kadmieli, wa Binui, wa Hodavia, 74. 44 Waimbaji wana wa Asafu; 148. 45 Waliofungua mlango wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni; wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai, 138. 46 Watumishi wa Hekalu wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi, 47 wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni, 48 wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Salmai, 49 wana wa wa Hanani, wana wa Gideli, wana wa Gahari. 50 Wana wa Reaya, wana wa Resini, wana wa Nekoda, 51 wana wa Gazamu, wana wa Uza, wana wa Pasea, 52 wana wa Besai, wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu. 53 Wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri, 54 wana wa Baslith, wana wa Mehida, wana wa Harsha, 55 wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema, 56 wana wa Nesia, wana wa Hatifa. 57 Wana wa Sulemani, wana wa Sotai, wana wa Sofeereth, wana wa Peruda, 58 wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli, 59 wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokerethi Sebaimu, wana wa Amoni. 60 Watumishi wote wa hekalu, na wana wa watumishi wa Sulemani, walikuwa 392. 61 Hawa ndio watu waliokwenda kutoka Tel Mela, Tel harsha, Kerub, Addon, na Imeri. Lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba wao au jamaa za baba zao walikuwa wana wa Israeli, 62 wana wa Delaya, wana wa Tobia, na wana wa Nekoda, 642. 63 Na kutoka kwa makuhani Wana wa Habaya, Hakosi, na Barzilai ( akamchukua mkewe kutoka kwa binti za Barzilai wa Gileadi na akaitwa kwa jina lao). 64 Hawa walitafuta rekodi zao kati ya waliojiunga na kizazi chao, lakini hawakuweza kupatikana, kwa hivyo waliondolewa katika ukuhani kama walio najisi. 65 Naye mkuu wa gavana akawaambia wasiruhusiwe kula chakula cha makuhani kutoka kwenye dhabihu mpaka atakapoinuka kuhani mwenye Urimu na Thumimu. 66 Kusanyiko lote lilikuwa 42, 360, 67 isipokuwa watumishi wao wa kiume na watumishi wao wa kike, ambao walikuwa 7, 337. Walikuwa na wanaume na wanawake wa kuimba 245. 68 Farasi zao zilikuwa 736 kwa idadi, nyumbu zao, 245, 69 ngamia zao, 435, na punda zao, 6, 720. 70 Baadhi ya wakuu wa familia za baba zao walitoa zawadi kwa ajili ya kazi. Gavana alitoa sadaka ya darkoni elfu ya dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 ya makuhani. 71 Baadhi ya wakuu wa familia za baba zao waliwapa katika hazina kwa kazi darkroni elfu ishirini za dhahabu na mane 2, 200 za fedha. 72 Watu wengine waliwapa darkoni za dhahabu ishirini elfu, na dhahabu elfu mbili za fedha, na mavazi sitini na saba kwa makuhani. 73 Basi makuhani, Walawi, walinzi wa malango, waimbaji, watu wengine, watumishi wa hekalu, na Israeli wote waliishi katika miji yao. Hata mwezi wa saba watu wa Israeli walikuwa wakiishi katika miji yao.”